UBAGUZI BAINA YA WAZAWA NA WAGENI WASEMEKANA KUKWAMISHA MAENDELEO MKOANI TANGA
Jamii Mkoani Tanga imetakiwa kuacha tabia ya
kibaguzi inayowagawa wazawa na wageni, badala yake washirikiane na kuwa kitu
kimoja katika shughuli za kimaendeleo.
Wakitoa maoni yao katika kipindi cha ASUBUHI YA LEO
kinachorushwa na kituo cha Pangani fm Radio, wachangiaji kutoka maeneo
mbalimbali ya mkoa wa Tanga, wamesema tabia hiyo ya kibaguzi ipo katika maeneo
mbalimbali ya nchi, huku wakisema tabia hiyo haifai kwani maendeleo ya wilaya,
mkoa na taifa ni jukumu la kila mmoja.
“Tunanyanyaswa
kisa sisi hatujazaliwa hapa, sio vizuri sisi ndio tunaleta chachu ya mabadiliko
ya iuchumi halafu wanatutenga, tukifanyikiwa kisa wageni wanatuibia si
utanzania huu, sisi tunahangaika kwa kuwa tunajua maendeleo ya wilaya zetu,
mikoa yetu na nchi yetu ni jukumu la
kila mmoja” wamesisitiza
baadhi ya wachangiaji.
Aidha wachangiaji hao wamesema kuwa ubaguzi huo unaoendelea
katika baadhi ya maeneo ya nchi, unaendelea kuwanyima baadhi ya watu na
kuwaweka tofauti watanzania jambo ambalo si utamaduni wa taifa hili.
“Mtanzania
si mgeni katika eneo lolote la taifa hata kama hajazaliwa eneo hilo, anazohaki
zote na anastahili kuzipata kama watanzania wengine aliowakuta eneo hilo.
Kwanini wanatugawa ndio utanzania huo”
wameendelea kusisitiza.
Katika hatua nyingine wachangiaji hao wameongeza
kuwa ni vyema serikali ikajiweka karibu zaidi na jamii, ili kujua masuala
mbalimbali yanayowasibu watanzania kila siku.
No comments