MAMLAKA YA MAJI PANGANI MJINI( PAWASA) INAWAOMBA RADHI WATEJA WAKE
Mamlaka ya maji Pangani mjini( PAWASA) inawaomba
radhi wateja wake kwa usumbufu kutokana na tatizo la kuharibika kwa mashine ya
kupandishia maji iliyopo kijiji cha Boza wilayani humo.
Akizungumza na Pangani fm, kaimu meneja mamlaka ya
maji Pangani mjini Bwana John Kisiwa Amesema kuwa kwa kipindi kifupi kutakuwa
na upatikanaji mdogo wa maji kutokana na hitilafu iliyojitokeza kwenye mashine
inayotegemewa.
“napenda kuuatarifu umma kuwa tumepata hitilafu katika mashine yetu kubwa ambayo tunaitegemea ya
uzalishaji maji pale boza
lakini jitihada kubwa zinafanyika
ili huduma hii iweze kurejea katika hali
ya kawaida hivyo tutakuwa na changamoto
ya upatikanaji wa maji kwa vipindi hivyo tunaomba radhi sana kwa wateja
wetu”alisema bwana kisiwa
Bwana kisiwa ameongeza kuwa kwa sasa mashine tayari
iko kwa fundi kwaajili ya matengenezo na
kusisitiza kuwa tatizo hilo litaisha kwa
muda mfupi pale matengenezo yatakapo kamilika.
“kwasasa
tumefanikiwa kuitoa ile mashine na tayari ipo kwa mtaalamu ambaye anaendelea kuishughulikia
sasa kiukweli hilo linategemea sana na
mtaalamu lini atatupa majibu tayari
amefanikisha lakini tunaamini ndani ya kipindi
kifupi tayari itakamilika na imeshasukwa
imekaa vizuri na huduma
No comments