KIFO CHA DIWANI SAIDI MAJIRA CHAACHA SIMANZI HALMASHAURI YA PANGANI
Halmashauri
ya Wilaya ya Pangani imeelezwa kusikitishwa na kifo cha aliyekuwa Diwani wa
kata Madanga Wilayani humo Ndugu Saidi Majira kilichotokea jana katika
hospitali ya Taifa Muhimbili.
Akizungumza
na Pangani fm Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Muheshimiwa Sefu
Ally Mapepo amesema kuwa "Ndugu Majira aliyekuwa akisumbuliwa na matatizo
mbalimba ilikwemo mgongo na kiuno alifikishwa Hospitali ya taifa na jana
akafariki dunia" ameleza MhSefu ally Mapepo
"Aidha Ndugu Saidi Majira pia alikuwa ni mshauri wa karibu wa Halmshauri kutokana na umahiri
wake katika kuongoza kamati mbalimbali, huku ikielezwa kuwa kuondoka kwake
kwenda mbele ya haki kumeacha pengo kubwa ndani ya Halmashauri hiyo."ameleza MhSefu ally Mapepo
Marehemu
Saidi Majira anatarajiwa kuzikwa hapo kesho majira ya saa saba mchana katika
kijiji cha Ushongo, huku wananchi wakitakiwa kuwa na subra katika kipindi hiki
kigumu cha kumpoteza mtu muhimu Ndugu Saidi Majira.
Shirika la
Uzikwasa na Pangani fm inatoa pole kwa wote walioguswa na msiba huu.
Innalillahi wainna ilayhi rajiuun- Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana
lihimidiwe.
No comments