WAKULIMA WILAYANI PANGANI WAJIPANGA KULIMA KILIMO CHA ALIZETI.
Kutokana na mabadiliko ya tabia nchi kuathiri uhakika
wa kupata mavuno ya kutosha kwa baadhi ya mazao wilayani Pangani wakulima
wilayani humo wamejipanga kuanzisha kilimo cha Alizeti ili kukabiliana na
athari hizo na kujikwamua kiuchumi.
Hayo yameelezwa na baadhi ya wakulima katika kijiji
cha Sange wilayani humo ambapo Bwana Albano Peter Mwalido amesema kwa sasa wao
kama wakulima wamehamasika kulima zao hilo kwakuwa limeonekana kuleta tija kwa
wakulima wa mikoa mingine nchini Tanzania.
‘’Zao
la alizeti mwanzo kabisa hatukuliwekea maanani na hata matumizi ya mafuta ya
zao hili hatukuwa tukiyatumia sasa dunia ni pana watu wamelikubali nje na ndani
ya wilaya yetu kilichobaki ni wakulima kuelimishwa namna ya ulimaji’’ amesema
peter.
Kwa upande wake mkulima Mwengine aliyejitambulisha
kwa jina la MATESO JOHN amesema wakulima
wengi katika wilaya ya Pangani wamechelewa kulima zao hilo kutokana na kuhofia kutostawi katika maeneo yao huku
akisema wakulima wengi wamejipanga kulima zao hilo kwa msimu ujao wa mwaka.
‘’Tangu asili
tulipokuwa tunakuwa tulikuwa tunaona wazee wetu wakilima ufuta, mihogo na
mpunga hili zao la alizeti tulikuwa tukilishuhudia kwa wenzetu tuu sasa tayari
kwa pangani limeonekana lina tija, ninachowaomba wakulima waongeze nguvu
yakulilima’’ amesema Mateso.
No comments