VIONGOZI WILAYANI PANGANI WAPATIWA MAFUNZO YA USIMAMIZI SHIRIKISHI WA RASILIMALI ZA BAHARI
Wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi kupitia mradi wa
SWIOFISH imetoa mafunzo kwa viongozi wilayani pangani yenye lengo la kuunda
jukwaa la wavuvi ili kusimamia na kushirikiana katika kulinda rasilimali za
uvuvi na kuangalia namna bora ya kuziwezesha kamati za BMUs wilayani humo.
Akizungumza katika mafunzo hayo muwezeshaji kutoka
wizara hiyo bwana TUMAINI CHAMBUA amesema kuwa kamati za BMU zipo kwa mujibu wa
sheria na zina tararibu zake hivyo ni vyema zijipange ili kuangalia namna ya
kupata mapato yatakayowezesha zijiendeshe na kufanikisha mapato ya halmashauri
zao.
‘’Kikao cha
wanachama wote ndo kinaweza kuamua hata zile sent mnazosema watu wapewe kile
kikao kinamaamuzi, ndo mana tunasema BMUs ifanye juhudi za kuona vyanzo gani
vya pesa na zikipata matumizi ya pesa wanaamuwa wenyewe kwenye vikao halali’’
asema tumaini
Wajumbe wa mafunzo hayo walipata nafasi ya
kuziwasilisha changamoto zao hususani katika ufuatiliaji wa uvuvi haramu
unaofanyika wilayani pangani huku wakizitaja changamoto zinazo wakabili
viongozi wa bmu ikiwemo suala la elimu ya kutambua majukumu yao.
‘’Ninachosisitiza
ni usimamizi wa sheria ndogo ndogo za BMUs, kama ni kiongozi awe ana meno ya
kuhakikisha usimamizi wa ukusanyaji mapato unasimamiwa ipasavyo, na kikubwa ni
elimu kwa viongozi wa BMUs ili viongozi watambue majukumu yao’’ hao ni baadhi
ya wajumbe wa mkutano huo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya
ya pangani muheshimiwa seif ally maarufu mapepo ameiomba wizara ya kilimo
mifugo na uvuvi kuzisaidia kamati za bmu kwa kuzipatia nyenzo ili ziweze
kujiendesha zenyewe.
‘’Wizara
ya kilimo,mifugo na uvuvi ni kubwa kuliko halmashauri, ninachoomba mimi ni
wizara kuzisaidia hizi kamati za bmu ili ziweze kujiendesha zipatiwe nyenzo’’ amesema
SEIF
Naye mratibu wa mradi wa SWIOFISH wilayani pangani
bwana HAMPHREY TILIA amesema kuwa watashirikiana kati aya BMU na wenyeviti wa
vijiji ili kukagua nyavu aina ya ringnet zinazotumika katika uvuvi wa maji
madogo ili kuzijua kuwa ni za halali au la huku akiongeza kuwa utekelezaji wa
kufutwa kwa usajili wa vyombo vilivyo kaa
zaidi ya miaka kumi na moja wanasubiri waraka kutoka wizara yenye dhamana ili
kuwapa muongozo kwa ajili ya utekelezaji huo.
‘’Tutashirikiana
bmu na wenyeviti wa vijiji tukakague hizi nyavu wawepo hao wavuvi tuende kwa
pamoja ili tujiridhishe hii nyavu kweli ringnet ya mchana ni ringnet kweli?
Inaruhusiwa kisheria? Kama inaruhusiwa kama hairuhusiwi tuiache ni nyavu
haramu.’’
Mafunzo hayo yaliyowashirikisha wenyeviti wa
halmashauri ya wilaya ya pangani, wenyeviti wa kamati za bmu, madiwani wa
halmashauri, wakuu wa idara ya mifugo na uvuvi huku yakiongozwa na mwenyekiti
wa halmashauri ya wilaya bwana seifu ali pamoja na mkurugenzi yamefikia tamati
kwa kuweka mikakati ya kuziwezesha kamati za bmu kuwa na miradi ya kimaendeleo,
kuzitatulia changamoto zao ikiwemo ukosefu wa vitendea kazi huku wizara ya
kilimo mifugo na uvuvi ikizipongeza kamati hizo kwa kazi nzuri ya ukusanyaji wa
mapato.
No comments