SHIRIKA LA UZIKWASA KURATIBU SHINDANO LA KAMATI BORA YA KUDHIBITI UKIMWI YA KIJIJI (VMAC),MWANAMKE BORA WA MFANO NA KIJANA BORA WA MFANO.
Shirikala uzikwasa limesema bado linaendeleo na
utaratibu wake wakuratibu mashindano makuu matatu ambayo ni kamati bora za kudhibiti
ukimwi za vijiji,mwanamke bora wa mfano wa kuigwa na kijana bora wa mfano wa kuigwa.
Hayo yamesemwa na
mratibu wa masula ya jinsia na uongozi wa shirika hilo BI SALVATA
KALANGA wakati akiwa katika kipindi cha subuhi ya leo kinachorushwa na kituo
hiki ambapo amevitaja baadhi ya vigezo
vya shindano la mwanamke bora .
“kigezo
cha kwanza tunamuangali mwanamke mwenye ujasiri na udhubutu wa kuhoji na
kuchangia shughuli zakimaendeleo,mwanamke mwenye uwezo wakufichua kutoa taarifa
na kufuatilia matukio ya kikatili na
unyanyasaji wa kijinsia unaofanyika katika jamii,mwanamke mwenye
kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kimaendeleo zinazonekana na
kutambulika si mwanamke anaekaa nyumbani
tu na kusubiri kupewa’’ aliendelea kutaja vigezo nyengine
ambavyo ni
‘‘mwanamke mwenye udhubutu na
kugombea nafasi mbalimbali za uongozi pindi zinapotokea ,na mwanamke anaetetea
haki za wanawake na za jamii kwa ujumla’’ alisisitiza BI SALVATA
Kwa upande wa shindano la kijana bora pia BI SALVATA
amevitaja vigezo na miongoni mwa vigezo
hivyo ni umri kati ya miaka 18 hadi 35 ambapo akivitaja vigezo hivyo
‘‘Awe
kijana anaeshawishi vijana wenzake katika sughuli za kimaendeleo,awe jasiri na kushiriki
katika nafasi mbalimbali za kiungozi,kijana asiye na makundi na anae
nyumbulika,na kwendana na wakati wa sasa katika kufichua na kufuatilia matukio
ya kikatili’’ aliendele kusisi tiza bi salvata kuwa
‘‘tumeweka kigezo hiki kwa lengo maalum kutokana na wimbi la matukio ya
kikatili yanayojitokeza na vijana wenyewe wanatajwa kuhusika ili kila kijana
awe anayafuatiia matukio hayo tuweze kuyatokomeza kwa pamoja ikiwa ni sambamba
na utoaji wa elimu kwa vijana wenzake’’Pia aliendelea kusisitiza kuwa
“hatumtaki
kijana ambae akisikia tukio lakikatili limetokea yeye anashangilia hatumtaki
kabisa kijana wa aina hiyo’’ ‘‘tunataka kijana mwenyeshughuli zake binafsi na anaejiingizia
kipatona si kijana anaekaatu maskani kuanzia asubuhi hadi jioni na kijana ambae
anahaiba nzuri mpaka kimavazi na si kijana anaevaa suruali chini ya makalia na
kunyoa kibuku.’’ Aliendeea kusisitiza bi salvata
Aidha bi salvata mesema ili kufanikisha mashindano
yote wanashirikiana na viongozi wa vijiji kwa kuvipa mamlaka vijiji kufanya
maamuzi katika kuwachagua watakaoingia katika mashindano hayo
No comments