WAKAZI WA KIJIJI CHA MTANGO WILAYANI PANGANI MBIONI KUPATA MAJI SAFI.
Mradi wa maji wenye thamani ya zaidi ya shilingi
milioni miatano na pwenti nane unatarajiwa kumaliza tatizo la maji kijiji cha
mtango kata ya mikinguni wilayani Pangani.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha mtango injinia
wa maji wilayani humo bwana NORBAT TEMBA amaesema tarehe 25 mwezi huu
wamemkabidhi mkandarasi mradi huo wa miezi sita ambao unatarajiwa kuanza mapema
tarehe 02/11/2017 na kukamilika tarehe 1/5/2018 ukiwa na vituo vya maji kumi,tank moja na mifumo ya kuvunia maji ya mvua mitatu.
Nae mwaeneyekiti wa halmashauri Mh SEIF ALLY (MAPEPO) amekiri kusaini mkataba
huo ambao pia una makubaliano ya kuwapa ajira zinazowastahili wakazi na vijana
wa eneo husika, huku akiwataka vijana kufanya kazi kwa bidii ili wajipatie
kipato kwa kipindi chote cha mradi.
Kwa upande wake Naibu waziri wa maji na umwagiliaji pia ni mbunge wa jimbo la Pangani Mh Jumaa Hamidu aweso amesema amefanya juhudi kubwa ili pesa hiyo
ipatikane huku akiwaomba vijana wa eneo hilo kufanya kazi katika mradi huo, pia
amemtaka mwenyekiti wa halmashauri kuangalia maslahi ya vijana watakaojitokeza
kufanaya kazi ili kuondokana na dhana ya kuwa vijana wa Pangani hawataki kazi.
Katika ziara hiyo Naibu waziri wa maji na umwagiliaji ameitaka halmashauri ya wilaya ya Pangani kuwahudumia wazee ipasavyo, asilimia 5 za kinamama na
vijana ziende kwa wahusika na zifike kwa wakati. pia ametaka kuwe na ushirikiano baina ya viongozi na wananchi
ili kuleta maendeleo kwa jimbo la Pangani.
No comments