WIZARA YA AFYA YAHAMASISHA MATUMIZI YA VYANDARUA KWA WANANCHI WA WILAYA YA PANGANI
Wizara ya afya maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na
watoto imetoa ujumbe kwa wakazi wa wilaya ya pangani mkoani tanga wenye lengo
la kuhamasisha matumizi ya vyandarua kuwa si kila homa ni malaria.
Akizungumza na wajumbe walioudhurika kikao cha
baraza la madiwani kilichofanyika wiki hii bwana MUSOBI KIYUNGU kutoka makao
makuu ya wizara ya afya (PSI) amesema kuwa nchi ya Tanzania imeazimia kumaliza
tatizo la malaria ugonjwa ambao unaongoza kwa kusababisha idadi kubwa ya
wagonjwa katika vituo vya kutolea huduma za afya na pia kusababisha vifo vingi vya watoto na watu wazima ambapo kampeni hiyo
imewalenga watoto, wakina mama wajawazito, na wazee.
Ameongeza kwa kusema kuwa kwa mkoa wa tanga wamepewa
wilaya nane na tayari zoezi la uhamasishaji limeanza maeneo ya tanga mjini,
mkinga na sasa wapo wilayani pangani na kuomba ushirikiano kwa maeneo ambayo
watapita ili kufanikisha zoezi hilo.
No comments