KIKUNDI CHA MAENDELEO VIKOBA MKWAJUNI WILAYANI PANGANI CHAGAWANA FAIDA.
Kikundi cha MAENDELEO VIKOBA MKWAJUNI kilichopo
katika kijiji cha MKWAJUNI kata ya UBANGAA leo kimefanya sherehe ya kumaliza
mwaka wa vikoba na kugawana faida.
Akizungumza katika sherehe hiyo Mgeni rasmi BI
VIKTORIA MFINANGA ambae pia ni afisa maendeleo kata ya mwera amewataka
wanakikundi hao kuzitumia pesa za faida walizogawana katika masuala ya
kimaendeleo huku pia akisisitiza jamii kujiunga na vikundi vya uzalishaji ili
kujipatia maendeleo.
‘’Tunaomba
wana mkwajuni mjifunze kutoka kwao kwa sababu ninaimani kuwa fedha
walizoziwekeza zitaenda kufanya kazi za kimaendeleo kwa hiyo kila mwana
mkwajuni anatakiwa kujiunga katika vikundi ili asaidie familia yake.’’ Amesema Bi Viktoria
Sambamba na hilo BI VIKTORIA amewataka wanakikundi
kuongeza ubunifu katika kubuni mradi wa pamoja na kushirikisha idara ya
maendeleo Wilaya ili kupatiwa mkopo kuletea maendeleo kikundi chao.
‘’kwamba sisi,
mtaji tutakao wapa hapa ni mkopo, muandae mradi wa pamoja na tutakuja uangalia
kama maafisa maendeleo ya jamii na tutawafanyia mchanganua wa huo mradi na
kuwapa mkopo wa asilimia 10’’. Ameelezea Bi Viktoria.
Kwa upande wake Katibu wa kikundi hicho BW MASHAKA
KABUPA amewataka vijana wa kiume kuhamasika katika kujiunga na vikundi vya
vikoba ili kujikwamua na kufikia malengo yao.
‘’mimi
kwa ujumla nina washauri vijana wenzangu kujiunga katika vikoba kwani ni vizuri
na vina faida. Hata mimi mwanzo nilikuwa sijajuwa faida yake na nikawa napanda
kwa kusuasua lakini sasa nimeona umuhimu wa vikoba’’ amesema Bwana Mashaka.
Kikundi cha MAENDELEO MKWAJUNI VIKOBA kwa sasa
kimetimiza mwaka mmoja huku kikiwa na wanakikundi 20 kati yao wanaume wakiwa 6.
No comments