WINGI WA AGENDA WASABABISHA MKUTANO WA KIJIJI CHA PANGANI MASHARIKI KUAHIRISHWA
Mkutano wa kijiji cha Pangani Mashariki jana
haukufikia tamati na hivyo kuahirishwa
kutokana na baadhi ya agenda kuonekana kutaka kujadiliwa kwa mpana na kupelekea
muda kutotosha.
Wakati wa ufunguzi wa mkutano huo afisa afya wilaya
ya Pangani Bwana JOSEPHAT MAKOMBE aliwasilisha hoja ya kutaka wananchi
wachangie ujenzi wa bohari ya dawa wilayani Pangani ili kupunguza changamoto ya
uhaba wa dawa.
‘’Ombi
kwa wananchi wote wa kijiji hichi, jitokezeni katika ujenzi wa bohari kuu ya
dawa, serikali ya awamu ya tano inajitahidi kupunguza tatizo la upungufu au
uhaba wa dawa kwenye vituo vyetu vya uhaba wa dawa’’ asema makombe.
Baadhi ya wanachi walihoji umuhimu wa Bohari hiyo ya
dawa,hali ya kuwa bado wanaendelea kununua dawa katika maduka binafsi ya dawa
mpaka sasa,ambapo bwana Makombe alitolea ufafanuzi.
‘’Faida
ya stoo hii nimezitaja kwamba zinatupelekea kupunguza tatizo la kukosa dawa
kwamba sasa dawa zitakuwepo wilayani kwetu pangani badala ya kwenda bohari kuu
ya dawa nchini’’ amefafanua makombe.
Kwenye wengi siku zote kuna mengi na mawazo ya
tofauti huwa yanaibuka,pengine wengi wanakubaliana na wazo la uwepo wa bohari
ya dawa ispokuwa kivipi kuwe na jengo wakati yapo yasiyotumika? Na hii ni hoja
binafsi.
‘’Jingo lipo,
halina kazi yeyote, hamlitumii, halmashauri hiyo hiyo alikuja mtu akataka lile
jengo kuliendeleza mkakataa bila sababu yeyote sasa kwa nini tunajenga jingo
jingine?’’ Alihoji mwananchi
Inawezekana kwa makofi hayo ni ishara ya watu
kukubaliana juu ya hoja hiyo,mkutano huo haukumalizika kutokana na muda kwani
wanachi walipata uwanda mpana wa kujadili masuala mbalimbali ambapo agenda
kama,suala la chakula shuleni,mradi wa ukarabati wa nyumba ya mwalimu katika
shule ya msingi Funguni,mojawapo ya agenda ambayo haikujadiliwa ni suala la
mapato ma matumizi ambalo litajadiliwa katikam mkutano utakaofuata.
No comments