KIJANA AATHIRIKA KISAIKOLOJIA BAADA YA KUNAJISIWA.
Picha hii sio ya kijana huyo.
Kijana mmoja wa kiume wa kijiji cha Kigurursimba (jina tunalihifadhi)
anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 22 amesema amefadhaishwa kwa kitendo
alichofanyiwa cha kuingilia kinyume na maumbile na mtu zaidi ya mmoja huku mmoja
wao akimfahamu kwa sauti hali
iliyosababisha kuathirika kisaikolojia.
Wakati akizungumza na Pangani fm Radio kijana huyo
alisema siku hiyo ya tukio alikuwa amelewa japo si sana ila mmojawapo wa vijana
waliomfanyia kitendo hicho cha kinyama alimfahamu kwa sauti.
’’ilikuwa
kama saa tano usiku nilipokuwa narudi nyumbani ambapo ni vijana zaidi ya mmoja
waliponiingilia nyumbani kwangu kwani nilisahau kufunga mlango na komeo hivyo
niliurudisha tu ndipo walipokuja na kuniingilia’’ amesema kijana huyo na
kuongeza.
’’kitendo
kilipotokea hata mimi mwenyewe nikawa kama sijielewi hivi kweli kijana kama
mimi ambae mpaka mtoto ninae halafu nafanyiwa kitu kama hicho basi nilikata tama kabisa na kupelekea kuhama kigurusimba na
kuja hapa mseko kuishi.’’alimalizia.
Kwa upande mwingine bibi wa kijan huyo anayeishi naye
kwa sasa Bi Asha Waziri alisema
‘’ baada
ya tukio hilo tulimpeleka hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu ambapo mara
baada ya hapo alionekana kama
ameathirika kisaikolojia kwani hata nyumba aliyoijenga mwenyewe aliamua
kuibomoa na kuhama kijijini hapo,ila sasa kilichokwamisha kuendelea kwa kesi ni
kwamba akili yake hata sasa haipo sawa kwa hiyo hata ushaidi hawezi kutoa kwa
sababu akili zake pia haziko sawa.’’
Kwa upande wake Mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya
pangani ambae pia ni kaimu wa jeshi la polisi wilaya BI MAYASA OMARI amekiri wao kama jeshi la polisi kupokea taarifa ya
tukio hilo ambalo lilitokea, pia amechukua nafasi hiyo kuiasa jamii kutoa
taarifa mapema pindi matukio hayo yanapotokea ili baadhi ya viashiria kwa ajili
ya ushahidi viweze kupatikana huku upelelezi juu ya tukio hilo ukiwa bado
unaendelea.
’’katika
tukio kama hili mtu inatakiwa siku ileile ambayo amefanyiwa tukio aripoti hata
daktari akimpima kuna viashiria vingi ambavyo tunavipata,sasa endapo zitapita
siku kadhaa basi tutafanikiwa kuangalia michubuko ambayo huacha weusi katika
sehemu hiyo ya haja kubwa,na hata sehemu yenyewe ya haja kubwa bado inakuwa wazi,
kwa hiyo alama zote hizi zinatakiwa kuthibishwa’’.amesema bi MAYASA
No comments