HOSPITALI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA PANGANI YAFANYA VIZURI KATIKA MPANGO WA MATOKEO MAKUBWA (B.R.N)
Hospitali ya Halmashauri ya wilaya ya Pangani
imefanya vizuri katika mpango wa matokeo
makubwa sasa (B.R.N)kwa kanda ya kaskazini kutokana na utendaji kazi mzuri wa
hospitali hiyo
Akizungumza na Pangani Fm Mganga mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya
Pangani Dokta KOMBO MHINA amesema kuwa
hivi karibuni wametembelewa na wasimamizi kutoka Wizara ya Afya ambao
hukagua utendaji kazi wa hospitali mbali
mbali nchini ambapo kwa hospitali hiyo wamepata nyota tatu na alama 72.
“Katika
hili tumejitahidi vyakutosha tunamshukuru
mungu hospitali yetu imepata
nyota tatu na alama 72 na kwa
mwaka jana tulipata nyota tatu pia lakini ilikuwa na alama 67 kwa hiyo tumebakiza point chache
tufikie alama za juu zaidi” alisema dokta kombo
Katika hatua nyingine dokta Kombo amesema pia wametembelewa na
usimamizi wa SAFE CARE kutoka Wizara ya Afya na mara baada ya kufanya ukaguzi
wao waliona kuwa wamefanya vizuri na kuwakabidhi zawadi ya ngao.
“Na
katika safe care baada ya ufanisi nakuonekana tunafanya tulipewa zawadi ya ngao na wawakilishi kutoka wizara
ya afya”alisema dokta kombo
Wasimamizi hao kutoka Wizara ya Afya huwa wanapita
katika hospitali mbali mbali nchini Tanzania ili kuona utendaji kazi wa
watumishi wa Idara ya Afya katika kutoa huduma kwa wananchi na kuangalia namna wahudumu wa afya wanavyojilinda na kuwalinda wagonjwa wasiweze kupata maambukizi yoyote.
No comments