VIJANA WASHAURIWA KUJIUNGA VIKUNDI ILI KUANZISHA MIRADI
Ziara ya mwenyekiti wa kijiji cha Boza kwa ajili ya elimu kwa wanchi juu ya namna ya
kujiunga katika vikundi mbalimbali vya kimaendeleo na ujasiriamali imeanza jana
katika kitongoji cha Choba.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa kijiji cha
Boza,Bwana Shabani Sufiani Musa na kuwataka wakazi wa kijiji cha Choba kuwa
katika vikundi kwa ajili ya kupewa mikopo ili kujiendeleza kiuchumi kwani
hakuna fedha yoyote ambayo serikali itaitoa kwa mtu mmoja pekee.
‘’Na
mradi ambao mtaubuni hakikisheni mnaandika na mahitaji yake ili mpate pesa
kulingana na namna ambavyo mnaweza kuuendesha,”tena sasa kuna wengine wamesema
hapa kwamba kipindi cha nyuma mlikuwa mnapewa pesa ambazo haziendani na
mahitaji sasa niwaambie kitu kimoja sasa hivi haitakuwa kama zamani mtu aomba
milioni moja anapewa laki mbili”alisema Shabani Sufian mussa.
Kwa upande mwingine afisa uwezeshaji wanachi kutoka
halmashauri ya wilaya ya Pangani Bi Ester John amewataka wanachi hao kuhudhuria
katika semina juu ya mafunzo ya ujasiriamali ambayo itafanyika katika kijiji
cha kimang’a tarehe 18 mwezi novemba mwaka huu 2017.
Semina hiyo itaendeshwa na wadau mbalimbali wa
maendeleo wakiwemo SIDO,watu wa benki akiwamo pia mkuu wa wilaya ya Pangani Bi
Zainabu Abdallah Issa.
Kijiji cha Boza kina vitongoji kama vile choba,mnazi
mmoja,kibaazi na Boza,ambapo ziara hiyo ni ya siku tatu,na huu ni utaratibu
ambao mwenyekiti huyo amejiwekea utaratibu wa kuzungumza na wanachi wake kwa
ajili ya kutoa mrejesho juu ya masuala ya uongozi na kuona namna gani ya
kutataua kero za wanachi.
No comments