VIONGOZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA PANGANI WATAKIWA KUTOWAKUMBATIA WAWEKEZAJI WASIO KUWA NA TIJA
Halmashauri ya wilaya ya PANGANI mkoani TANGA
imetakiwa kuacha kuwakumbatia wawekezaji wasio na tija katika shughuli za
kimaendeleo, badala yake wapewe nafasi watakayoweza kuleta mabadiliko ya
kiuchumi.
Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani hapo
jana mkuu wa wilaya ya pangani bi ZAINAB ABDALLAH ISSA, amesema kuwa duni
kiuchumi kumechangiwa na halmashauri kuendelea kuwakumbatia wawekezaji wasio na
tija, huku akisema idadi kubwa ya wawekezaji katika halmashauri hiyo kwa kiasi
kikubwa wamekuwa wakikwepa kushiriki katika ajenda za kimaendeleo
Bi zainab
amesema wawekezaji waliopo katika halmashauri hiyo wanamanufaa makubwa
wanayoyapata kutokana na rasilimali zilizopo, ilhali manufaa hayo kwao ni bure
kwa jamii.
‘’hatuna uwekezaji wenye tija tunawatu kama amboni,
hivi kweli wanatulipa milioni 10 kwa mwaka? Wanachangia nini? Tuna kituo cha
afya mwera na hiki ndo kituo tegemezi kwa upande wa ng’ambo na watu ni wengi
kuliko huku, tunaomba basi mtusaidie kumalizia hiki kituo’’
Aidha bi zainab ameongeza kuwa pamoja na halmashauri
kuzungukwa na rasilimali za kutosha ikiwemo fukwe za bahari, bado haionekani tija
ya wawekezaji waliowekeza maeneo hayo, ambapo mkuu huyo ameendelea kusisitiza na
kutoa onyo kali kwa waheshimiwa madiwani kutosahau majukumu yao.
‘’uwekezaji kwenye mahoteli, tuna fukwe mwanzo mpaka
mwisho wa mipaka yetu, rasilimali za kwetu wanazozitumia,,, sasa wataalamu
jamani mnatushauri nini? Kweli wanatunufaisha hawa watu? Ifike mahala tuwe na
wawekezaji wenye tija’’
Mwanzoni mwa mwaka huu waziri wa nchi ofisi ya rais
tawala za mikoa na serikali za mitaa muheshimiwa SULEIMANI JAFFO alipokuwa
ziarani wilayani pangani alipata nafasi yakuzungumza na wakuu wa idara,
madiwani na wananchi katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo huku akitoa agizo
kwa mkurugenzi wa amboni plantaion tawi la mwera kusaidia ujenzi wa thieta katika
kituo cha afya mwera na pia alionekana kushangazwa na vitendo vya wawekezaji
katika halmshauri ya pangani kuonekana kutokuwa na msaada kwa wanajamii wa
wilaya hiyo.
hayo yameibuka katika baraza la madiwani october 30/2017
No comments