WANANCHI WILAYANI PANGANI WATAKIWA KUNYWA DAWA ZA NGIRI MAJI NA MATENDE ILI KUTOATHIRI UKUAJI WA UCHUMI.
Wananchi Wilayani Pangani wameshauriwa kushiriki
kikamilifu katika zoezi la unywaji wa dawa za magonjwa yaliyokuwa hayapewi
kipaumbele, zoezi ambalo limekwishaanza kutekelezwa kwenye maeneo yote wilayani
humo.
Akizungumza mapema leo katika kipindi cha ASUBUHI YA
LEO kinachorushwa na kituo hiki Mratibu wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi
kipaumbele Wilayani Pangani Dk Yusuf Makange, amesema kuwa kuendelea kusambaa
kwa magonjwa hayo kunaendelea kuathiri uchumi wa nchi kutokana na nguvu kazi
kubwa ya taifa kuugua.
‘’Mbwu
amekuwa ni msafirishaji wa magonjwa kutoka kwa mtu kwenda kwa mtu mwingine
ambapo athari zake mtu anavimba sehemu za siri, anakuwa na tende na matokeo
yake anapata ulemavu.’’amesema dokta makange.
Aidha Mratibu huyo wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi
kipaumbele Wilayani Pangani amesema kuwa, Pangani ni miongoni mwa halmashauri
tano mkoani Tanga zenye kiwango kikubwa cha maambukizi ya magonjwa hayo, huku
akiwaomba viongozi mbalimbali kutumia nafasi zao kuhamasisha wananchi wao ili
kufanikisha zoezi hilo.
‘’Halmshauri
tano mkoa wa tanga bado tunaendelea na hili zoezi kwa sababu maambukizi yapo
juu, kwa hali hiyo ndo mana tunasisitiza kuwa viongozi waliokuwepo katika ngazi
nikimaanisha mwenyekiti wa kijiji hadi viongozi wote maarufu tunaomba
ushirikiano katika hili ili kuondoa maambukizi’’amesema dokta makange.
No comments