WAKAZI WILAYANI PANGANI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA YA VIWANDA VIDOGO VIDOGO
Shirika la kiserikali linaloshughulikia viwanda
vidogo (SIDO) limetembelea Wilayani pangani ili kuwapa elimu wananchi wa wilaya
hiyo kuwatambua namna wanavyofanya kazi na kutoa hamasa ya uundaji wa vikundi
ili waweze kunufaika.
Akizungumza na wadau wa maendeleo wilayani humo Afisa
uendelezaji biashara na kaimu meneja
kutoka shirika hilo bi GLADNESS FOYA amesema lengo la shirika hilo ni
kuendeleza technolojia na ufundi kwa wajasiriamali wadogo ili waweze
kujiendeleza kiuchumi.
‘’Tunasaidia
wajasiria mali wadogo ili kuona namna gani wataweza kuendeleza technolojia ya
viwanda vidogo na namna gani wataweza kupata mashine mbali mbali kwa bei nafuu
ili waweze kuanzisha biashara zao. Lakini tunatoa vifaa mbali mbali kwa mafundi
wadogo wadogo kama vile mafundi vyarahani, ujenzi na fundi kapenta’’ amesema
foya.
Amesema kuwa kupitia vikundi vya vijana, sido
inauwezo wakuwaandaa ili waweze kujua namna ya kuchakata na kutengeneza bidhaa
zitokanazo na ngozi na kuwataka wadau hao kutoa ushirikiano ili kufanikisha
swala la viwanda vidogo vidogo.
‘’ Bado tunalenga kwenye hili soko kwa vijana wa
shule ili kuona kwa namna gani wanaweza kutengeneza chaki ili ziweze kuwasaidia
katika swala la ufundishaji lakini bado tunaweza kuwatumia vijana waone namna
ya kuchangamkia fursa ya utenngenezaji wa viatu kwa kutumia ngozi, hili ni moja
ya soko litokanalo na viwanda hivi vidogo’’
No comments