VIJANA WILAYANI PANGANI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIMAENDELEO.
Vijana Wilayani Pangani wametakiwa kuchangamkia na
kuzitumia fursa mbalimbali zilizopo na zinazojitokeza ili kujikwamua na
kuyafikia malengo yao.
Akizungumza akiwa katika mafunzo ya ujasiriamali kwa
vijana eneo la Pangani mjini mkuu wa Wilaya hiyo BI ZAINABU ABDALAH ISA
amewataka vijana wenye ujuzi kuchangamkia fursa ya ujenzi wa bomba la mafuta
kutoka hoima nchini UGANDA hadi Tanga nchini TANZANIA huku akiahidi kuwasaidia
vijana hao ili kupata nafasi za ajira.
‘’ niwaombe
vijana kuna nafasi za kazi kwenye bomba la mafuta mkoani tanga kwa hiyo vijana
ambao wana ujuzi na wanahisi kuwa huenda wakatumika nipate cv zao wazilete
kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya’’ amesema mkuu wa wilaya Bi Zainabu.
Wakiwa katika warsha ya mafunzo ya ujasiriamali
vijana wa Pangani mjini walipata nafasi ya kuwahoji viongozi wao juu ya masuala
mbalimbali yanayowahusu ambapo Bwana SWAHIBU MWANYOKA alitaka kujua utayari wa
halmashauri katika kuwafanya vijana kuyatumia maeneo ya bichi.
‘’Vinaja
wengi tatizo mitaji hakuna lakini wanafikra za kufika mbali sasa mkurugenzi
kupitia halmashauri yake atueleze kuwa halmashauri ipo tayari kuwapa vijana
maeneo ya beach ili kujipatia kipato ili kuiongezea halmashauri mapato?’’
alihoji mmoja kati ya vijana.
Akitoa ufafanuzi juu ya swali hilo kaimu mkurugenzi
wa halmashauri ya Wilaya ya Pangani amewatoa hofu vijana hao kwa kusema kwa
sasa halmashauri iko tayari kuwaelekeza vijana maeneo ya bichi ili vijana hao
waweze kufanya shughuli za kijasiriamali.
‘’kwanza niseme kuwa kama kijana anafanya miradi
yake ya ujasiriamali sisi hatutakuvunjia ila tutakuelekeza sehemu sahihi ya
kufanya hizo biashara zako na mwisho wa siku pangani iwe bora hasa katika
kuwavutia watalii’’ amesema kaimu mkurugenzi bwana ARCHI MATAMBO.
Mafunzo ya ujasiriamali na zoezi la uundwaji wa
majukwaa ya vijana yataendeleo katika kata zote zilizopo ndani ya Wilaya ya
Pangani huku kesho ikiwa ni zamu ya kata ya Mkalamo na Mkwaja.
No comments