HATIMAE KAMATI ZA BMU WILAYANI PANGANI ZAANZA KUPOKEA MALIPO YAO

Hatiame halmashauri ya Wilaya ya Pangani leo imeanza zoezi la kuzilipa kamati za BMU baada ya kamati hizo kukaa miezi 6 bila malipo.

Akizungumza katika kikao na kamati hizo kabla ya kuanza kwa zoezi la malipo kaimu mkurugenzi wa halmashsuri ya Wilaya ya Pangani BW ARCH MTAMBO amezihakikishia kamati za BMU zote kupata malipo yao kama inavyotakiwa.

‘’naomba niwaaminishe kwamba hakuna shilingi ya bmu, ambayo imekuja kwa ajili ya bmu ambayo itapotea, kama ambavyo leo mtalipwa fedha zenu basi mjiwe kila pesa zitakapo patikana mjuwe mtalipwa bila shida’’ amesema bwana Arch.

Mara baada ya kikao hicho lililofuata  ni zoezi la kutembelea vitalu vya miti ya mikoko iliyooteshwa  na BMU hizo kwa lengo la kuheshabu miti iliyofikia katika hatua ya upandaji  huku changamoto kubwa ya iliyoibuliwa na kamati hizo ni wadudu aina ya chago wanaokata miti hiyo.

‘’Taarifa zetu tulizozileta zilieleza wazi kuwa humu kulitakiwa kuwe kama pale, lakini matatizo yamekuja huku kuna chago, na taarifa tumekuletea hii tumepanda tangu mwezi wa tano mwaka huu lakini haiwezi kustawi kwa sababu hiyo kama tutalipwa kwa miche haiwezekani,’’amesema mmoja wa bmu.

Baada ya mivutano na utaratibu wa kuhesabu miche kukamilika utaratibu wa malipo uliandaliwa ambapo kamati za BMU kijiji cha bweni na Pangani mashariki zimekwishapokea malipo yao.

‘’tunashukuru bmu yetu ya bweni tumefanikiwa kupata fedha zetu tulizokuwa tunaidai halmashauri jumla zote ni milioni tatu na laki tano lakini kutokana na miche kutotimia hatukufanikiwa kuzipata fedha zote’’ amesema mmoja wa bmu.

Kwa upande wake BW ARCH MTAMBO ambae ni kaimu mkurugenzi amezitaka kamati hizo za BMU kujipanga kwaajili ya kuutumia ukingo wa bahari unaoendelea kujengwa katika ene o la Pangani mjini.

‘’Wilaya yetu ya pangani watu wengi watataka kuja kujifunza sasa ninachowaomba tusiwe wachoyo wa kutoa hii fursa kwa wengine na tuendelee kutunza vitalu vyetu kwani vitatusaidia kupata miche mingi ya mikoko ambayo itakuwa mwanzo mzuri wa utunzani wa ukingo wetu’’ amesema arch.

Kamati za pangani magharibi inatarajia kupokea malipo yake hapo kesho baada ya utaratibu wa malipo kukamilika.

No comments

Powered by Blogger.