KIJIJI CHA PANGANI MASHARIKI CHA PIGA MARUFUKU UUZAJI WA CHAKULA ENEO LA MAGALAWANI
Serikali ya kijiji cha pangani mashariki imepiga marufuku
uuzwaji wa vyakula katika
eneo la magarawani
na badala yake wafanyabiashara
hao waende katika maeneo maalum waliopangiwa.
Akizungumza na pangani fm kwaniaba
ya mwenyekiti wa kijiji hicho
bwana SALIMU KIRABA ambaye ni mwenyekiti
wa kitongoji cha funguni alisema kuwa
hali ya usafi katika eneo linalouzwa
haliridhishi kiafya hivyo
nivema kutii agizo la kuhamia
katika eneo maalum waliotengewa.
“huu
niutaratibu kwa wale wote ambao
tuliwapa viwanja vya kufanyia
biashara hali iliyofikia ni tete
nimefika kwa mama mmoja pale nikakuta amepika chakula
mbele kama hatua mbili kuna jalala hapa anapopika
chakula hatua kumi kuna choo ...na
bahati nzuri mama huyo aliwahi kupewa
onyo na maafisa wa afya kwamba asifanye
biashara katika eneo hilo kwa hiyo nasema wasije kutulaumu viongozi”alisema
kiraba
Aidha
bwana KIRABA mbali na kusisitiza
wafanyabiashara kuhama katika
eneo hilo amesema kuwa serikali
imetenga eneo juu kidogo na hilo (eneo la pangadeko) kwaajili wa wanaofanya bishara kwa kuwa
nisalama kiafya hali ambayo itaepusha magonjwa ya mlipuko .
“hili
tuliliona na ndio maana tuliwatengea maeneo ma
kwa sababu huwezi kuuza na
chakula wakati mwenzio anachemsha uono ,uono una mambo mawili unatoa maji na unamwaga damu
hapo nzi hawawezi kukosekana nzi
atatoka hapo aende kwenye andazi la mteja
ndio mana tukasema wafanyabishara wajenge katika maeneo husika”alisema
kiraba
Hayo yamejiri
baada ya wataalamu afya kutembelea
eneo hilo na kutoridhishwa na hali ya
usafi iliyopo na kushauri uongozi
wa kijiji kuwatengea eneo
maalum wafanyabishara hao
No comments