GARI KUACHA NJIA NA KUTUMBUKIA MTO PANGANI.
Gari moja aina ya MITSUBISH-CANTER yenye namba za
usajili T 336 AAE mali ya Bwana MRISHO HEMEDI BAKARI, limeacha njia na
kutumbukia katika Mto Pangani eneo la CASTAM palipo na Bandari ya Pangani.
Akithibitisha tukio hilo Mkuu wa Polisi Wilaya ya
Pangani Bi Christina Musiani amesema kuwa tukio hilo limetokea leo Desemba Mosi
2017 majira ya saa Tano na Nusu Asubuhi, baada ya kondakta wa gari hilo Ally
Hemedi mwenye umri wa miaka 23 alipokuwa akiligeuza gari hilo mara baada ya
kumaliza kupakua Machungwa waliyokuja nayo kutoka Wilayani Muheza.
Aidha Mkuu huyo wa Polisi Pangani amesema kuwa
pamoja na ajali hiyo kutosababisha madhara yoyote kwa Binaadamu, imesababisha
uharibifu wa gari hiyo huku kijana Ally Hemedi ambaye ni Kondakta wa gari hilo
akitokomea kusipojulikana hadi sasa.
“Leo desemba mosi gari aina ya Mitsubish
Canter T 336 AAE imeacha njia na kutumbukia katika mto pangani eneo hilo la
Kastam ilipo Bandari ya Pangani baada ya kondakta wa gari hili alipokuwa
akiligeuza mara baada ya kumaliza kupakua machungwa waliyokuja nayo kutokea
Wilayani Muheza ili aweze kulipaki vizuri tayari kwaajili ya kuondoka”
“Pamoja
na kusababisha uharibufu katika gari hilo tunashukuru Mwenyezi Mungu ajali hiyo
haikusababisha madhara yoyote kwa binaadamu, tayari gari hiyo imeshatolewa na
iko kituoni kukaguliwa na taratibu nyingine za kisheria zinaendelea, na kijana
Ally Hemedi ambaye ni Kondakta wa gari hilo ametoroka hatujui amekimbilia wapi
hadi sasa’ amesema Mkuu wa Polisi Pangani Bi Christina Musiani.
Katika hatua nyingine Bi Musiani ameongeza kuwa
wakati wote Madereva wa vyombo vya moto wanapaswa kuwa makini, huku akitoa wito
kwa madereva wote kupunguza Mihemko ya Mwisho wa Mwaka akisema baada ya Mwaka
kumaliza, kuna Mwaka Mpya unaokuja hivyo maisha ni lazima yaendelee.
“Wakati
wote lazima wazingatie usalama wa barabarani, tunapoendesha vyombo vya moto
tusiangalie ufaghari au umaarufu Fulani kwamba unaweza kukimiliki chombo cha
moto, lakini kikubwa ni kuangalia kwamba vile vyombo vimetengenezwa na binaadamu
na wewe unahitaji kuishi” Amesema Bi Musiani na kuongeza kuwa
“Kwa
hiyo madereva tuthamini sana nafasi tulizopewa kuishi na tuwe makini kwa
kufuata sheria za barabarani, pia mihemko ile ya mwisho wa mwaka tuipunguze
kwasababu baada ya mwaka kuisha tunauanza mwaka mwengine lazima maisha
yaendelee tuzingatie na tuwe makini katika matumizi ya barabarani” Amesisitiza Bi
Musiani.
Katika eneo hilo la KASTAM ilipo Bandari ya Pangani
ni mara ya kwanza ajali kama hiyo kutokea, ambapo tukio hilo limezua taharuki
kwa wapita njia pamoja na wapakiaji na wapakuaji mizigo eneo hilo.
No comments