MHESHIMIWA AWESSO MGENI RASMI TAMASHA LA VMAC KESHO PANGANI
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji nchini ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Pangani Mheshimiwa Jumaa Hamidu Awesso amefanya ziara katika kituo cha redio Pangani Fm na kuthibitisha kuhudhuria katika tamasha la VMAC linalotarajiwa kufanyika kesho katika kijiji cha Msaraza wilayani Pangani.
Akizungumza katika mahojiano maalumu yaliyofanyika jioni ya leo, Mhehsimiwa Awesso mbali na kufarijika kupewa mwaliko wa kuhudhuria tamasha hilo, pia amelisifia shirika la UZIKWASA kwa kazi zake nzuri za kuelimisha jamii ya Pangani na kupaza sauti za wanyonge.
"Kwa kweli mtu atayelipinga shirika la UZIKWASA atakuwa halitendei haki, mimi toka nipo mdogo nalisikia shirika hili kazi zake, pia kupitia Pangani Fm wananchi wameweza kupaza sauti zao kiasi cha kero nyingi za kimaendeleo kutatuliwa" alisema Mheheshimiwa Awesso.
Naibu Waziri huyo wa Maji na Umwagiliaji aliambatana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Pangani Bwana Chambasi Damiani ambaye pia alieleza maendeleo ya uchimbaji wa kisima cha maji katika kijiji cha Masaika.

No comments