SHIRIKA LA UZIKWASA LAKUTANA NA WADAU WA ELIMU PANGANI
Shirika La Uzikwasa lililopo wilayani Pangani limekutana na kuzungumza na baadhi ya
wadau wa elimu kwa kwa ajili ya kupata mrejesho wa utekelezaji wa shughuli
mbalimbali zinazofanywa na shirika la Uzikwasa kwa kushirikiana na wadau hao.
Akizungumzia kuhusu mafanikio waliyofikia Mwenyekiti
wa Kamati ya shule ya msingi Kwakibuyu Bwana SAMWELI DENIS amesema kuwa
wamejitahidi kutatua changamoto mbalimbali kama vile ya uchache wa walimu kwa
kushgirikisha wadau wa elimu waliopo katika eneo hilo.
‘’Nafikiri
kuna mambo tumeyafanikisha kuna mambo bado kwa sababu yapo kama mambo manne au
matano yaani kuna kuwepo kwa kujitahidi kuwepo chakula shuleni, nyumba za
walimu, ujenzi vyoo na tumeongea na uongozi wa amboni plantation na yapo baadhi
ya majengo wameyakarabati’’ amesema Samweli.
Aidha kutokana na mfumo salama wa kuripoti matukio
ya ukatili kwa watoto bwana Samweli amesema wamelazimika kugawana majukumu na
wajumbe wa kamati yake kufuatilia
matukio ya ukatili kwa watoto.
‘’Mfumo
tumetengeneza kwa sisi wenyewe wana kamati kwamba kama utasikia jambo ufuatilie
wewe mwenyewe kimnywa kimnywa na baada ya hapo tunaitisha kikao na kujadili ili
tuangalie namna ya kulifanyia ufumbuzi kwa ujumla’’ amesema Samweli.
Kwa upande wake Mwezeshaji kutoka shirika la
Uzikwasa Bwana Kennedy Mashema amesema zoezi limekwenda vizuri huku miongoni
mwa makubaliano katika zoezi hilo ni kamati Kutembeleana, kufuatilia Kesi za
ukatili kwa mfumo salama na kuchukua hatua stahiki.
‘’Katika kutathimini utendaji wa wadau imekuja
ikaonekana kwamba kuna masuala inabidi yaangaliwe kwa kina kwa mfano
ushirikiano kati ya kamati na walimu kwa maana ya matroni na patroni ili tuone
namna ambavyo wanaweza kutatua matatizo ya kijinsia, sasa kuna matukio mengi
sana ya ukatili kama shirika tukaona namna bora ya kuyapata ni kuweka huu
mtandao wa uripotiji matukio’’ amesema Kennedy.
Zoezi la kukutana na wadau wa elimu wilayani
Pangani litaendelea leo kwa kanda ya
kaskazini ya mto Pangani ambapo wawezeshaji hao watakutana na wadau katika
kijiji cha Msaraza.
No comments