MVUA YASABABISHA TAMASHA LA VMAC KUTOKUFANYIKA KIJIJI CHA PANGANI MASHARIKI
Tamasha la Ukimwi, Jinsia na Uongozi
lililokuwa lifanyike jana kijiji cha Pangani Mashariki katika uwanja wa Kiwanda
cha Makumbi limeshindikana kufanyika
kutokana na hali ya mvua na iliyokuwa inanyesha mfululizo
Akizugumzia kuhusu hali hiyo
Mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana HAJI NUNDU
amesema wamelazimika kuahirisha Tamasha hilo kutokana na wakazi wa
kijiji hicho kutofika katika sehemu iliyopangwa kufanyika tamasha hilo hali
aliyoitaja kusababishwa na mvua.
‘’Tulipanga kufanya tamasha katika
uwanja huu wa kiwanda cha makumbi lakini hali ya hewa ni ya mvua ambapo hata
watu hawaja jitikeza na hata Yule tuliyempanga kwa ajili ya mziki naye anasema
mziki wake ni mbovu na ndio maana tumelazimika kuhairisha mkutano huu’’ Amesema
Nundu.
Aidha Bwana Haji Nundu amesema baada
ya kuahirisha leo tamasha hilo wanatarajia kulifanya siku ya Ijumaa wiki ijayo katika sehemu hiyo
huku akiwataka wakazi wa kijiji hicho kuhudhuria kwa wingi siku hiyo ili
kushughudia yale walioibua katika mafunzo ya Jinsia na Uongozi kijijini hapo.
‘’Sasa tujipange mungu akituwezesha
siku ya ijumaa ijayo tutafanya tena tamasha hili, ninachoomba watu wajitokeze
kwa wingi ili kufanikisha tamasha letu.’’ Ameongeza Nundu.
Tamasha la jinsia na uongozi hufanyika siku nne baada ya wajumbe wa kamati
ya kudhibiti ukimwi jinsia na uongozi
kupata mafunzo kwa siku tatu mfululizo ambapo wahusika katika onyesho la
igizo ni wajumbe wa kamati husika iliyopatiwa mafunzo.
No comments