MSHINDI WA VMAC PANGANI KUJILIKANA KESHO
Wakazi wilayani pangani wamealikwa kufika kwa wingi
katika tamasha la kupata kamati bora ya kudhibiti ukimwi jinsi na uwongozi kwa
mwaka 2017 litakayofanyika katika kijiji
cha Msaraza kata ya Bushiri kesho siku ya Jumamosi ya tarehe 16/12/2017.
Akizungumza mapema hii leo na Pangani Fm Mwwezeshaji
kutoka shirika la uzikwasa Bi Salvata Kalanga amesema wakazi wilayani Pangani
wasisubiri kusimuliwa bali wafike kwani kujione yale yatakayojiri,huku shughuli
hiyo ikitarajiwa kuanza saa tatu kamili asubuhi.
‘’Nipende katika kuwaalika watu wote ambao katika
mchakato mzima wa kumtafuta mwanakamati bora wa kamati ya jinsia na uongozi ,
kesho ni tamati ya tamasha hili ambalo lilikuwa likisubiriwa na watu wengi wamekuwa na kiu ya kuwa nani ataibuka kidedea
na ninaomba mtu asisubiri kuambiwa na mwenzake basi asogee mwenyewe ili
ajionee’’ amesema Salvata
Bi Salvata ameongeza kwa kusema maandaliza ni mazuri
huku akitanabaisha kuwa shughuli nzima
itapambwa na burudani kutoka kwa wasanii wanaotaka katika maeneo mbali mbali
kutoka wilaya ya Pangani
‘’Tutakuwa na burudani ambazo zinatoka ndani ya
wilaya yetu, kutakuwa na muziki, ngoma za asili na mgeni rasmi tumeshampata na
naamini atakuwa pamoja nasi, kwa ujumla maandalizi yako mazuri karibuni wote’’
ameongeza Salvata
Kwa upande wake Bwana Kenedy Mashema ambaye ni mwezeshaji
kutoka shirika la Uzikwasa amawaalika watoto wote wiliopo katika wilayani
pangani kufika katika Kijiji cha msaraza
ili waweze kuona shirika la uzikwasa linavyowapigania haki zao na huku akiongeza
kuwa kwa wale watakao shindwa kuhudhuria
wategea sikio Pangani Fm radio.
‘’watoto wote kwa wilaya ya pangani mnatakiwa
kuudhuria, kama hautaweza kufika katika tamasha letu basi ni vyema ukatega
sikio pangani fm radio ili uweze kumsikiliza motto mwenzako ambaye ni balozi wa
watoto kwa waliya ya pangani na ataelezea maswahibu yanayowakuta watoto’’
amesema Keneddy.
Shindano hilo kwa mwaka huu limebeba kauli mbiu
isemayo “Lisilowezekana, Linawezekana”
No comments