MHESHIMIWA AWESSO AWATAKIA HERI YA KRISMASS NA MWAKA MPYA WANANCHI WA JIMBO LAKE

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Pangani Mheshimiwa Jumaa Hamidu Awesso wamewatakia sikukuu njema ya Krismass na mwaka mpya wa 2018 wananchi wa jimbo lake huku akisisitiza suala la amani na usalama.

Akizungumza na Pangani Fm kwa njia ya simu jioni ya leo, Mheshimiwa Awesso amesema kuwa mbali na suala la usalama kuanza kwa mwananchi mwenyewe, lakini pia ni vyema kutoa taarifa kwa vyombo vya husika ili kila mwananchi asherehekee sikukuu kwa amani.

"Napenda kuwatakia heri ya sikukuu ya Krismass na Mwaka Mpya wanachi wa jimbo langu la Pangani, kikubwa ninachowaomba katika sikukuu hizi ni kuhakikisha suala la usalama, kwa sababu usalama unaanza na mwananchi mwenyewe, na ikitokea mtu anavunja amani, ni vyema kuripoti kwa mamlaka husika, nina imani wamejipanga vyema" alisema Mhehshimiwa Awesso

Mheshimiwa Awesso pia ametumia wasaa huo kutoa tahadhari kwa watumiaji wa ufukwe wa bahari ya Hindi hususani wageni, ambapo mbali na kuwataka kuheshemu mila na utamaduni wa Pangani katika kujisitiri, pia amewataka kuwa makini na kuepukana na vifo visivyo vya lazima wakati wakiogelea.

"Jambo jengine ni kuwa, nitoe tahadhari kwa wageni wote watakaokuja kutembelea ufukwe wa bahari ya Hindi hususani eneo la Pangadeko, kwanza wafuate utaratibu za usalama kwa maeneo ya kuogelea ilim kuepukana na vifo ambavyo vinaweza kuzuilika, na pia waheshimu utamaduni wetu wa Pangani, naomba wajisitiri ili kuepuka kuwakwaza wenyeji" alisema Awesso.

Tahadhari hiyo kutoka kwa Mheshimiwa Mbunge Jumaa Awesso imekuja siku mbili baada ya jeshi la polisi wilayani Pangani, kutoa tahadhari kama hiyo kwa lengo la kudhibiti masuala ya uhalifu na kulinda amani hasa katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu ya Krismass na Mwaka Mpya.



No comments

Powered by Blogger.