MSHINDI WA VMAC 2017 PANGANI KUJULIKANA DISEMBA 16
Hatimae mchujo wa mwisho wa kutafuta kamati bora za kudhibiti ukimwi, Jinsia na Uongozi umefanyika leo katika ukumbi wa Safari Annex huku kamati mbalimbali zikiwasilisha taarifa zao.
Akizungumza mara baada ya mchujo huo mmoja wa majaji waliokuwa wanasimamiza zoezi hilo Bwana Novatus Urassa amesema kuwa, mchakato huo umekwenda vizuri na kila kamati imewasilisha taarafa yake kama walivyotarajiwa na kilichobaki sasa ni kusubiri kilele cha kumtangaza mshindi.
Bwana Urassa pia amesema kuwa, mashindano hayo kwa mwaka huu 2017 yatarajiwa kufanyika katika kijiji cha Msaraza kata ya Bushiri wilayani Pangani mnamo tarehe 16 ya mwezi huu siku ya jumamosi
Urassa ameweka bayana kuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ya kumtangaza mshindi ni Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaji Mheshimiwa Jumaa Hamidu Awesso.
Mbali na kuipata kamati bora ya kudhibiti Ukimwi, Jinsia na Uongozi pia siku hiyo atatangazwa mshindi wa kijana bora wa mfano, pamoja na kijana bora wa mfano wa kuigwa hasa katika masuala ya kimaendeleo.
Shindano hilo kwa mwaka 2017 limebeba kauli mbiu isemayo "YASIYOWEZEKANA, YANAWEZEKANA"

Nawatakia maandalizi mama ya sherehe hizo
ReplyDeleteTunashukuru sana Abdul kwa kuendelea kutufatilia.
Delete