UZIKWASA YAKUTANA NA WADAU WA ELIMU KIJIJI CHA MSARAZA WILAYANI PANGANI
Wadau wa maendeleo ya elimu na vita ya kupinga
ukatili wa kijinsia waliokutana na wawezeshaji kutoka Shirika la Uzikwasa
katika Kituo cha Msaraza wameonyeshwa kuwa na Imani na jitihada zinazofanywa na
Shirika hilo katika kupinga masuala ya Ukatili wilayani Pangani huku wakiomba
jitihada zaidi kufanyika ili kuondoa masuala ya ukatili.
Wakizungumza katika zoezi la kuwakutanisha wadau hao
wamesema wanaunga mkono juhudi zinazofanywa na Shirika la Uzikwasa ambapo
matunda yameanza kuonekana utokana na vita dhidi ya masuala ya Ukatili huku
wakishauri kuongezwe zaidi jitihada kwa kufikisha mada za ukatili kama ajenda
katika mikutano ya kijiji inayofanyika kila baada ya miezi Mitatu.
‘’Suala la ukatili katika wilaya ya pangani
tunatakiwa tutoe elimu ya kutosha katika kamati za vijiji ili tufikie malengo
na tufikie hatua tutokomeze, elimu kubwa inatakiwa kupelekwa pia katika kamati
za shule ili tupate matunda mazuri baada ya miaka miwili’’ amesema mmoja wa wadau.
Nae Makamu Mwenyekiti wa kamati ya shule ya Msaraza
Bwana IDD MAZIKA amesema kutokana na mafunzo ya Minna dada yamesaidia kwa kiasi
kikubwa katika kuimarisha mahusiano mema kati ya wazazi, walimu na kamati
pamoja na viongozi wa dini hali iliyopelekewa kufanikiwa kupunguza utoro kwa
wanafunzi pamoja na kufanikiwa kutia sakafu katika baadhi ya vyumba vya
madarasa katika shule ya msingi Msaraza.
‘'Mimi nichukulie mafunzo ya halafu camp yameleta
mabadiliko makubwa kwa vijiji vyetu mwanzo kabisa hakukuwa na cheini ya
ushirikiano lakini kwa sasa cheini imekuwa nzuri kati ya wazazi, walimu na
jamii na hata taasisi za lijamii, ukipata tatizo au changamoto yeyote
ukiwatafuta wadau wa maendeleo yaani haichukui muda unatatuliwa changamoto yako
hakika mafunzo ya alafu camp yamesaidia’’ amesema Mazika.
Katika hatua nyingine kutokana na kupata mafunzo
kuhusu mfumo salama wa kuripoti matukio ya ukatili dhidi ya watoto wadau hao
wameelezea yale waliofanikiwa kuyafuatilia na kuelezea mikwamo wanayokutana
nayo.
‘’Kesi ilikuja kwa mwenyekiti wa kitongoji na
tukamwambia hizi ni hatua za kisheria na tutafuata taratibu za kisheria kwa
kuanza kumpeleka mtuhumiwa wetu polisi. Amesema Mjumbe.
Kwa upande wake mwezeshaji kutoka shirika la
uzikwasa bwana Nikson Lutenda ameelezea kufarijika kwa namna wadau hao
walivyoelezea maendeleo yao baada ya mafunzo kutoka shirika hilo huku akisema
watafanyia kai mapendekezo walioyapata ili kutokomeza masuala ya ukatili
wilayani Pangani.
‘’Kwanza katika maeneo ambayo nimevutiwa zaidi
katika kijiji hichi cha msaraza ni viongozi wake wamefunguka zaidi katika
kusikia uchungu, mjumbe na mwenyekiti wote wameonekana kuguswa na matatizo
yanayowakabili wanafunzi, nimependa pia mahusiano yanayojengwa kati ya kamati
ya shule na wazazi, kikubwa ni shirika la uzikwasa tuwe nao pamoja wadau katika
kuendesha gurudumu hili la elimu’’ amesema Nickson.
Zoezi la kukutana na wadau wa maendeleo ya elimu na
vita ya kupinga masuala ya ukatili wa kijinsia hufanyika kila baada ya miezi
sita Kwa ajili ya kutathimini utekelezaji wa shughuli mbalimbali zinazofanywa
na shirika la Uzikwasa kwa kushirikiana na wadau hao wa elimu.
No comments