WANANCHI WILAYANI PANGANI WAOMBWA KUJITOKEZA KATIKA MDAHALO WA TAKUKURU



Wakazi wilayani pangani wametakiwa kuudhuria kwenye mdahalo utakaofanyika December 12 ili kujadili masuala mbali mbali yatakayoweza kuzuia na kupambana na rushwa katika kuadhimisha siku ya maadili na haki za binadamu kwa mwaka 2017.

Wito huo umetolewa na mkuu wa TAKUKURU wilaya ya pangani Bwana JOSEPH PAUL wakati wa mahojiano na Pangani Fm radio na kusema kuwa kuna namna ya kutoa taarifa kupitia simu ya mkononi pale ambao umeona mtu anatoa au kupokea rushwa.

‘’Nitiwe wito kwa watu wa pangani wajitokeze kwenye mdahalo pale katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya pangani ili tuweze kupata muafaka wa kukomesha vitendo vya rushwa’’ amesema Joseph.

Ameongeza kwa kusema kuwa mfumo wa sheria katika masuala ya rushwa ilipaswa kuwepo sheria kali ili kuwawezesha wala rushwa hata kufungwa endapo watakutwa na hatia kutokana na suala hili kuathiri uchumi wanchi.

‘’Huu mfumo wa sheria katika haya masuala ya rushwa kwa sababu tunajuwa haya makosa ya rushwa yanahasiri uchumi wa nchi, kungekuwa na sheria kali zaidi watu wangeogopa kutenda makosa haya’’ Amesema Joseph.

Maadhimisho hayo yanafanyika leo tarehe 10 disemba kwa ushirikiano wa taasisi za serikali zinazosimamia maadili, uwajibikaji, utawala bora, haki za binadamu na mapambano dhidi ya rushwa.

No comments

Powered by Blogger.