WAZAZI WILAYANI PANGANI WASHAURIWA KUWEKEZA ELIMU KWA WATOTO WAO
Wazazi na walezi wilayani Pangani wameshauriwa
kuwekeza kwa watoto kielimu kwa
kuwasomesha bila kuwabagua kijinsia kwa kuwa watoto wote ni sawa lakini
kipaumbele kiwe kwa watoto wa kike.
Akizungumza
na wazazi waliohudhuria kwenye mahafali ya sita shule ya msingi MAKORORA
wilayani humo Mhifadhi kutoka hifadhi ya Taifa SAADAN Bwana ROMANUS MKONDA amesema elimu ndio urithi pekee
kwa mtoto
‘’Somesheni watoto bila kuwabagua kama huyu ni wa
kike au wa kiume lakini mimi nawashauri muwekeze zaidi kwa watoto wa kike, na
sio kuwasubiri wamalize elimu yao ya msingi na kuanza kuwapeleka katika kazi za
housegirl’’ amesema Mkonda.
Naye diwani wa viti maalum Mkwaja Bi HADIJA MAKATA amewataka
kinamama kubadili mtazamo kutoka kwenye kununua mavazi na kuwekeza katika
elimu.
‘’Kwa hiyo mama, mtoto anapomaliza shule na kufaulu
vizuri kaweke rehani Madera ili mtoto aendelee na masomo kwa sababu sasa hivi
elimu haichangishwi chochote ni bure kabisa, nawashauri wazazi wenzangu
tufanyeni bidii katika kuwawezesha watoto kielimu na kama mtoto amefaulu
hujataka kumsomesha nitahakikisha tunakwenda sambamba’’ amesema Bi Hadija.
Katika suala la mahusiano mazuri kati ya wazazi na
walimu Katibu wa chama cha walimu CWT wilayani humo Mwl Ibrahim Mayunga amewataka wazazi na walimu kuwa na ushirikiano
ilikuleta maendeleo nchini.
‘’Sasa zile zama za kale tuziache, zamani mwalimu
kama mwalimu alionekana ni mgomvi na jamii na ilitokea katika baadhi ya shule
sijui kata ya mkwaja, mwalimu akiwa anafundisha kuna mwingine analinda nyumba
za walimu je kuna mwizi? Hizi ni zama ushirikiano kati ya walimu, wazazi na
jamii kwa ujumla tushirikiane kuhakikisha mtoto anapata elimu ya uhakika’’
amesema mwalimu.
Licha ya shule yamsingi MAKORORA kukabiliwa na changamoto
ya uhaba wa walimu na madarasa shule HIYO imepanadai kitaaluma ambapo kwa mwaka
2016 imekuwa ya 4 kiwilaya huku mwaka 2017 ikishika nafasi ya 3 ikiwa na
wanafunzi 12 waliofanya mtihani na kufanikiwa kufaulisha wanafunzi kumi watano
wakike na wengine watano wakiume.
No comments