UKATILI WA KIJINSIA KUPELEKEA KASI YA MAAMBUKIZI YA VVU
Imeelezwa kuwa ukatili wa kijinsia umekuwa kichocheo kikubwa cha ongezeko la maambukizi
ya vvu katika jamii.
Hayo yamesemwa na BW NOVATUS URASA ambae ni makamu
mkurugenzi wa shirika la Uzikwasa lililopo Wilayani pangani wakati dunia ikiwa
katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia
BW URASA amesema kuwa hapo awali shirika la uzikwasa
lilikuwa likitoa elimu zaidi kwenye masuala ya ukimwi lakini kwa sasa
limejikita katika kutoa elimu juu ya tabia hatarishi na matukio ya ukatili wa
kijinsia yanazopelekea maambukizi ya VVU na kuwawezesha viongozi kuchukua hatua
ili kupunguza kasi ya maambukizi kwani vitu hivyo vinakwenda sambamba.
“ukatili wa kijinsia kwa kiasi kikubwa sana umekuwa
ukichangia maambukizi ya vvu,sisi kama shirika la uzikwasa hapo awali tulikuwa
tukitoa elimu hasa katika masuala ya vvu lakini baadae tukagunduua kuwa
kuielimisha jamii juu ya ukimwi bila ya kuielimisha jamii juu ya masuala ya
ukatili wa kijinsia ni sawa na bure kwani kwa sasa watu
wanabakwa,wanalawitiwa,
wanapigwa na kuwaathiriwa kisaikoljia hii imekuwa
ikipelekea mwenza kuamua kutafuta faraja popote jambo ambalo wakati mwingine
mtu huyo anaweza kuingia sehemu yoyote akiitafuta faraja bila kufikiria madhara
take na kujikuta kupata maambukizi"
Adha BW URASA amewataka watanzani kuendelea kuchukua
tahadhari dhidi ya VVU na kuacha tabia yakupuuza uwepo wa janga hilo.
“Ukimwi bado upo ,vvu bado ipo maambukizi yako pale pale ukimwi
haujasafisi ila ni kama watu wamejisahaulisha ,ujumbe tunaoutoa kupitia
maadhimsho haya tunashauri tahadhari ziendee vile vile kama zilivyokuwa
zikitolewa katika kipindi ambacho watu walikuwa wakiuzungumza sana na wale
wanaopata maambukizi waendelee kuhudumiwa kama
kawaida,unyayapaa usiwepo na
jamii ijiepushe zaidi na ukimwi”
Tarehe mosi mwezi desember kama leo kila mwaka dunia
huadhimisha siku ya ukimwi na katika Wilaya ya pangani maadhimisho hayo
hanafanyika katika kijiji cha Mkaramo.
No comments