USHIRIKIANO SIRI YA MAFANIKIO VMAC KIJIJI CHA KIMANG'A WILAYANI PANGANI
Ushirikiano baina ya Wananchi, viongozi na Kamati ya
Kudhibiti Ukimwi Jinsia na Uongozi ya kijiji cha Kimang’a umeelezwa ndio siri
pekee iliyosababisha kamati hiyo kuingia katika orodha ya kamati kumi na saba
bora mwaka 2017.
Akizungumza na PANGANI FM Mjumbe wa kamati hiyo
Bwana Selemani Hamisi, amesema kamati yao katika shindano la kamati bora mwaka
2015 ilishika nafasi ya 33 ambayo ni ya mwisho kati ya kamati 33 za vijiji vilivyopo
Wilayani pangani, jambo ambalo liliwafanya kujipanga upya na sasa kuingia
katika orodha ya kumi na saba bora.
Aidha Bwana Selemani ameongeza kuwa kamati hiyo
imekuwa ikifanya kazi kwa Umoja na Ushirikiano bila kuangalia undugu, hasa
katika kushughulikia matukio ya Ukatili wa Kijinsia.
Katika hatua nyingine Katibu msaidizi wa kamati hiyo
Bwana DAUDI BUSHISHI amesema kuwa kamati hiyo itaendelea kuwajibika hata kama
haitapata nafasi tatu za juu katika shindano la kamati bora na wala hawatakata
tamaa.
‘’Tukikosa
nafasi yeyote katika kamati lazima kama wanakamati wa kijiji cha kimang’a
tutakaa ili tujipange upya na kuangalia namna bora ya kuweza kupata nafasi za
ushindi, kwa mi ninavyoona mwaka 2015 tulishika nafasi ya 33 na kitu na kwa
mwaka jana tukashika nafasi ya 22 na mwaka huu tumeingia 17 bora kwa hiyo
tukikosa nafasi hivyo vitu havitawezekana ni lazima tupige vita vya ushindi’’ Amesema
Bushishi.
Tarehe 12 mwezi huu kamati za kudhibiti Ukimwi
Jinsia na Uongozi za vijiji Wilayani Pangani, zinatarajiwa kufanyiwa mchujo wa
mwisho na hatimae kupata kamati bora zilizofanya vizuri zaidi katika
utekelezaji wa mipango kazi yao kuanzia January 2017.
Kauli mbiu ya shindano hilo mwaka huu “inasema
(yasiyo wezekana yanawezekana)
No comments