"MFUME DUME UNAZOROTESHA MIPANGO YA MAENDELEO KWA WANAWAKE" BI HALIMA
Kuendelea kukumbatiwa kwa Mfumo Dume
Wilayani Pangani kumeelezwa kusababisha mikwamo na changamoto za kiungozi kwa
wanawake, pasi na kuangalia ujasiri na uwezo wao katika kufanikisha mipango ya
kimaendeleo.
Akizungumza na kituo hiki Bi Halima
Hamisi ambaye ni mshindi aliyeshika nafasi ya tatu katika shindano la kutafuta
mama bora wa mfano wa kuigwa Wilayani Pangani 2017, amesema kuwa mwanamke
anapojiamini anaweza kufanya mengi yenye faida kwenye jamii yake, lakini baadhi
ya watu kuendelea kuukumbatia mfumo dume kunasababisha kufinika uwezo walionao.
Aidha Bi Halima amesema kuwa katika
uwezo wake mumewe anahusika kwa kiasi kikubwa kwani ni tofauti na wanaume
waliowengi, akimsifu kwa kumtia moyo na uvumilivu alionao.
“Kwa kweli suala la Uongozi Wilayani
Pangani, tena sijui niseme mkoa wote wa Tanga! Yani changamoto ni nyingi lakini
nashukuru nipo na mume anayejitambua, laiti ningekuwa na mume asiyejitambua
sijui ingekuwaje. Ila nashukuru mume wangu anajitambua ni mume anayejielewa,
ukweli kwa hilo napenda kumshukuru sana. Ananiunga mkono ni mwanaume mvumilivu
sana” amesema Bi Halima.
“Mwanamke ukijiamini unaweza na usipo
jiamini kila siku utabaki kuwa nyum. Mimi nimejiamini na kweli nimeweza kwani
hata nilipochaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya shule nilifanikisha
upatikanaji wa maji shuleni tatizo ambalo kwa muda mrefu liliwatesa wanafunzi,
pili nilisimama kidete na kulishughulikia tatizo la vyoo shuleni hapo na hadi
sasa ukiachilia vyoo, kuna madarasa mawili ya kisasa pale shule ya msingi
mivuni ukifika utayaona mazuri”amesisitiza Bi Halima Mama Bora Wilayani Pangani
2017.
Pamoja na hilo amegusia changamoto
nyingine inayomkabili kama mkwanamke ni itikadi za kisiasa akisema amewahi
kuondolewa kwenye nafasi ya uongozi katika kamati ya maji kutokana na
kutofautiana na wengine kiitikadi, lakini bado amehakikisha kukazana akisema
yapo mengi kwenye jamii yanayopaswa kushughulikiwa.
“Kweli hilo ndio linalotuathiri
mivunoni, unapokuwa wewe ni mwanachama wa chama kingine, utatafutiwa mbinu za
kila aina, watu wanaunda visababu, hata katika uongozi utatolewa tu hilo ni
lazima yani hapa nasema wala sifichi, mimi kule kwenye kamati ya maji
nimetolewa bila sababu ya msingi lakini bado nakazana na mengine kwani kwenye
jamii yapo mengi yanayopaswa kushughulikiwa. Amesema Bi Halima.
Amemalizia kwa kuwashauri wanawake
wengine kujitambua na kutobaki nyuma, wala kuogopa watu wanasemaje badala yake
wahakikishe wanaondoa tofauti zao nakushikamana kuijenga jamii kwa pamoja.
“Ushari wangu kwa wanawake wenzangu kwa
kweli tujitambue, na utakapotambua kuwa wewe ni mwanamke na unaweza usibaki
nyuma na wala usiogope kwamba yule atasemaje! kwani mti unaopigwa mawe ni
mzuri, kwa hiyo wote inatakiwa tuheshimiane, tukubaliane, tufanyekazi kwa
pamoja, kwani tukishaanza kuleta ukwanini hatutajenga mana sisi wote ni jamii
moja, tuondoe zile tofauti za ukwanini” amesema Bi Halima.
Bi Halima Hamisi ni mwenyeji katika
kijiji cha Mivumoni Wilayani Pangani, ambaye ameshika nafasi ya tatu kama mama
bora wa mfano wa kuigwa 2017 katika shindano la kutafuta kamati bora ya
kudhibiti ukimwi jinsia na uongozi VMAC-Kijana Bora na Mama Bora wa Mfano wa
kuigwa kwa mwaka 2017, tamasha lililofanyika katika kijiji cha Msaraza Wilayani
humo Desember 16 mwaka huu.
No comments