WANANCHI PANGANI WATAKIWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA KUTEKELEZA MIPANGO INAYOWEKWA NA SERIKALI
Jamii Wilayani Pangani imeombwa kushiriki kikamilifu
katika juhudi mbalimbali za kutekeleza mipango inayowekwa na serikali na hata
mashirika binafsi kwa ajili ya kupinga mabadiliko ya tabia nchi.
Hayo yamesemwa na katibu tawala mkoa wa Tanga Bi Zena
Ahmed Saidi alipohudhuria katika uzinduzi wa mradi wa mabadiliko ya tabia nchi
ambapo amesema kuwa, serikali inafanya jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya
tabia nchi hivyo wananchi nao nijukumu lao kuchukua hatua ili kukabiliana na
mabadiliko hayo.
‘'Kwa
hiyo katika kukabiliana na hili tumeona serikali imejenga ukuta na nyinyi kama
wananchi muelekeze nguvu zenu katika hili suala la upandaji wa mikoko ili
kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi’’ amesema Zena.
Awali akiwasilisha taarifa ya Mradi Afisa kutoka
shirika la Climate Action Network Bwana Kelvin amesema kuwa matarajio yao kama
CAN ni kuwaongezea wadau uwezo kuhusu namna bora ya kukabiliana na kujenga
ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.
‘’Kuwaongezea wadau kuhusu namna bora ya kukabiliana
kujenga ustahamilivu dhidi ya athari za mabadiliko ya tabia nchi, kupunguza
uharibifu na upotevu wa vitu mbali mbali kutokana na athari za mabadiliko ya
tabia nchi, kupunguza uharibifu na upotevu wa vitu mbali mbali nah ii ni
kutokana na kikao kilichokaliwa huko Poland kwa ajili ya mpango wa kuwasaidi
wananchi wan chi zinazoendelea. Amesema Kelvin.
Kutokana na mabadiliko ya tabia nchi kumuathiri
mwanamke moja kwa moja katibu tawala wa mkoa Bi Zena amelisisitiza shirika la CAN
kumtumia kwa asilimia kubwa mwanamke ili waweze kufanikiwa katika mradi wao.
‘’Kwenye mawasilisho yenu mlikuwa mnasema kuwa
mwanamke ndio wanaopata shida sana endapo kutatokea mabadiliko ya tabia nchi
kwa sababu kama ni maji wao ndo watafuata huduma hiyo kwa umbali zaidi, sisemi
kama wakina baba hawaathiriki hapana, sasa kutokana na hilo ni vyema katika
hali ya kupambana na mabadiliko haya ya tabia nchi ni vyema mkawashirikishwa
wanawake kikamilifu pia msiwasahau wakina baba’’ Amesema Zen.
Mradi huu wa uunganishaji jitihada za kukabiliana na
athari za mabadiliko ya tabia nchi maendeleo endelevu pamoja na kupunguza
umasikini nchini Tanzania, umezinduliwa leo katika wilaya ya pangani na mradi
huu utatekelezwa kwa kipindi cha miaka 3 katika wilaya mbili za mkoa wa Tanga
ambazo ni Lushoto na Pangani pamoja na wilaya ya Chalinze mkoa wa Pwani, huku
ikizishirikisha sekta za kilimo, mifugo, uvuvi,
mazingira, ustawi wa jamii, maliasili na nishati.
No comments