WANAWAKE KIJIJI CHA PANGANI MASHARIKI WATAKIWA KUWEKA KIPAUMBELE KATIKA KUTETEA HAKI ZAO.
Wanawake wa Kijiji cha Pangani Mashariki Wilayani
Pangani wametakiwa kuwa kipaumbele katika kutetea haki zao, na kujiona wana uwezo
wa kushika nyadhfa mbali mbali za uongozi kwenye Jamii zao.
Akizungumza wakati akiendesha mafunzo ya Jinsia kwa
kamati ya kudhibiti Ukimwi, Jinsia na Uongozi VMAC ya kijiji cha Pangani
Mashariki, muwezeshaji kutoka shirika la Uzikwasa Bi Salvata Kalanga, amesema
wanawake lazima wajitambue na wadai haki zao ili kujiletea maendeleo wao
binafsi na jamii nzima kwa ujumla.
‘’Tutakapofikia
kwenye suala la kudai maendeleo, wanawake lazima tudai haki zetu, hatuko katika
zama za kale, kwa hiyo wanawake lazima tufuke maali tuwe na lugha
zitakazotufanya tusikilizwe, na ndio maana mafunzo haya hatuyatoi kwa wanawake
peke yake, tunawachanganya ili tutembee katika njia moja’’ amesema Salvata.
Nao baadhi ya wanaume waliopo kwenye kamati hiyo
walikuwa na mitazamo tofauti kuhusu kumpa uwongozi mwanamke katika nyanja mbali
mbali, huku wakisema wamekuwa wagumu
kuwapa wanawake uwongozi kwa sababu ni rahisi kurubuniwa.
‘’Wanawake wamekuwa na udhaifu mwingi sana na hata
kwenye kurubuniwa ni raisi, mimi kama mimi katika maisha yangu sitaki mwanamke
aniongoze hawa watu hawana misimamo kabisa’’ amesema mmoja wa wanaume hao.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Pangani
Mashariki Bwana HAJI NUNDU amewataka wajumbe wanzake kuyathamini mafunzo hayo
na kuyapeleka katika jamii zao, ili kuondokana na mikwamo mbali mbali
inayowakabili katika jamii yao.
‘’ La msingi na la busara ni kufanya thamani ya
mafunzo haya ili tupunguze au kuondoa kabisa suala la unyanyasaji.’’ Amesema
HAJI NUNDU
Haya yamejiri leo katika siku ya pili ya mafunzo
wanayopatiwa wajumbe wa kamati ya kudhibiti Ukimwi, Jinsia na Uongozi ya kijiji
cha Pangani Mashariki, mafunzo yenye lengo la kuibua matukio ya ukatili,
unyanyasaji kwa wasichana pamoja na wenza ili kuyatafutia ufumbuzi wa pamoja.
No comments