UNESCO YAIPONGEZA PANGANI FM KWA HABARI ZA MITANDAONI


Shirika la UNESCO nchini Tanzania limekipongeza kituo cha radio jamii Pangani Fm kinachomilikiwa na UZIKWASA kwa kazi nzuri ya kutimia blog kwa lengo la kupasha habari zitokanazo na jamii wanayoifanyia kazi.

Pongezi hizo zimetolewa na afisa ufuatiliaji na tathmini Bwana  MARKO G SHEKALAGHE wakati wa mafunzo ya ufatiliaji na tathmini kwa vipindi vya redio yaliyofanyika kwa muda wa siku tano mkoani Iringa.

Wakati wa mafunzo hayo Bwana SHEKALAGHE alikitaja kituo cha Pangani Fm kama mfano wa kuigwa na redio nyengine za kijamii kwa kuwa habari wanazoweka kwenye blog yao zinaakisi jamii ya watu wa chini.

"Muige wenzenu wa Pangani Fm, habari zao zote ni zile zinazotoka maeneo ya kijijini, kama hamjui, sisi tunaokaa mjini, tunataka sana kujua habari vijijini, pale ofisini tukikaa, huwa tunatembelea sana blog ya Pangani Fm kwa kuwa wanatoa habari za Pangani tu" Alisema SHEKALAGHE

Mbali na hilo Bwana SHEKALAGHE alimuomba muwakilishi kutoka kituo cha Pangani Fm ambaye alihudhuria mafunzo hayo Bwana Mohammed Hammie kueleza habari hiyo ya mafanikio kwa Bi Luiana Temba kutoka shirika la UNESCO ili kuwa chachu ya mafanikio ya pamoja yaliyotokana na mafunzo yanayotolewa na shirika hilo.

Pangani Fm ilianza kutoa habari zake kwa njia ya Blog mwezi wa nane mwaka 2017 baada ya kuwezeshwa kwenye mafunzo ya ICT na shirika la UNESCO,  ambapo imejikita zaidi kutoa habari za vijijini pekee ili kuleta utofauto na blog nyengine zenye habari zinazofanana,  unaweza kutembelea blog hiyo kwa kuandika www.panganifm255.blogspot.com

1 comment:

Powered by Blogger.