"UKOSEFU WA TAARIFA SAHIHI NI HATARI WAKATI WA UJAUZITO" DOKTA MAGIRI
Ukosefu
wa taarifa sahihi za mimba katika kipindi chote cha ujauzito kupitia kadi ya
Clinic, kumeelezwa kusababisha hatari ikiwemo kifo kwa mama au mtoto
anayetarajiwa kuzaliwa.
Hayo
yamesemwa na Daktari MAGIRI EMILY kutoka kitendo cha Wodi ya Wazazi katika
Hospitali ya Wilaya ya Pangani wakati akifanya mahojiani na kituo hiki, na
kuongeza kuwa Jamii Wilayani humo inapaswa kufuatilia na kufahamu umuhimu wa
kadi ya Clinic ya Uzazi, ili kuepuka madhara yatokanayo na uzazi.
Aidha
amewashauri wazazi kujipanga katika suala la ujauzito ili kuikabili hali hiyo,
hivyo ameshauri namna bora ya kuilea mimba hadi mama atakapojifungua salama.
“Kwa jamii kikubwa kinachotakiwa kuzingatia ni
kujipanga, wazazi wajipange kwenye masuala ya ujauzito, mama anapokuwa
majamzito basi wazazi wote wawili wajipange kwani mimba sio ugonjwa bali ni
sehemu ya maisha yetu wanadamu, kwa hiyo wajipange kikamilifu kwa namna ya
kuielea hiyo mimba na namna ya jinsia mama atakavyojifungua salama” amesema Dk
Magiri.
Daktari MAGIRI amesema lengo la kutoa elimu
hiyo kwa jamii ni kutokana na takwimu zao kuonyesha kiasi kikubwa cha jamii
kupuuza vidokezo vilivyopo ndani ya kadi hilo kitendo kinachoweza kusababisha
madhara makubwa kwa wajawazito, hivyo anatumai ya kwamba elimu hiyo itasaidia
kuongeza uelewa katika jamii juu ya umuhimu wa kadi hilo.
“Tumependa
kutoa hili somo kwa jamii kufahamu umuhimu wa hii kadi kwa maana ya kuzuia
matatizo ya wajawazito, hii ni kutokana na takwimu zetu kwenye hospitali pamoja
na vituo vyetu vinavyotoa huduma za uzazi tumeona kwamba wazazi wengi wanakuja
hawajali vile vidokezo vilivyowekwa pale. Kwa hiyo lengo la sisi kama wataalam
kutoa elimu hii ni kupunguza matatizo yanayojitokeza kwa wamama na watoto
wanaozaliwa” amesisitiza Dk Magiri.
Daktari
huyo kutoka wodi ya wazazi katika Hospitali ya Wilaya ya Pangani amemalizia kwa
kusema kuwa lengo lao kwa mwaka 2018, ni kuona idadi kubwa ya wanajamii
wanaojua umuhimu wa kadi hilo na kulitumia ipasavyo, ili kuepuka madhara kwa
mama mjamzito na mtoto anayetarajiwa kuzaliwa kwa kuhakikisha wanakuwa salama.
No comments