WANANCHI WILAYANI PANGANI WAMETAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA NCHI.
Wananchi wilayani Pangani wametakiwa kuzingatia sheria
kwa kuzijua pamoja na kuzitii ili ziwape muelekeo wa utatuzi wa matatizo
yanayowakabili.
Hayo yamezungumzwa na mwanasheria wa wilaya ya
pangani bwana BARICKEL MSAKI wakati wa mazungumzo maalumu na pangani fm na kusema kuwa iwapo mtu atazingatia sheria za
nchi atakuwa na uwelewa juu ya sheria hizo na atatambua pia namna ya kuzifanyia
kazi.
‘’Wito mkubwa ni kuzingatia sheria kwa sababu
ukizingatia sheria utaepusha kujiingiza kwenye mikono ya sheria kwa maana
kwamba sheria zinasemaje kwa kuzingatia utiii wa sheria bila shuruti’’.amesema
barickiel
Ameongeza kwa kusema kuwa pale ambapo mwananchi
ametokewa na matatizo yanayoitaji masaada wa kisheria ni vyema akawatafuta
wanasheria kwa wakati ili kuwasaidia kuwapa ushauri utakaowawezesha kutatua
matatizo yao.
‘’Pale wanapotokewa na matatizo yanayoitaji kupata
usaidizi wa kisheria kwa wakati ni vyema wakawatafuta wanasheria ili wapate
usaidizi wa sheria kwa haraka’’ amesema tena msaki.
Hayo yamekuja kufuatia maadhimisho ya wiki ya msaada
wa huduma za kisheria ambayo hufanyika kila mwaka ambapo kwa mwaka huu kilele
chake ni kesho December 8 huku yakibeba kauli mbiu isemayo ‘’umuhimu wa utoaji
wa haki kwa wakati kuwezesha ukuaji wa uchumi.
No comments