MAMLAKA YA MAJI PANGANI MJINI YAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA MHESHIMIWA AWESSO
Siku moja baada ya agizo la Naibu Waziri wa Maji
na Umwagiliaji Mheshimiwa Jumaa Hamidu Awesso kuitaka Mamlaka ya maji Pangani Mjini
(PAWASA) kuwa hadi kufikia leo tarehe 5/12/2017 upatikanaji wa
maji uwe umetengemaa eneo la Pangani Mjini, hatimae mamlaka hiyo tayari imeanza kuchua hatua za utekelezaji.
Akizungumza na Pangani Fm mapema leo meneja wa maji
Pangani Mjini Bwana Adamu Sadick amesema kuwa wamepokea agizo hilo la Naibu Waziri wa Maji
kwa moyo mmoja, na mpaka sasa wanalifanyia kazi na wako katika hatua za mwisho za
matengenezo na kuwataka wananchi wilayani Pangani kuwa na uvumilivu juu ya
tatizo hilo.
‘’Tumepokea agizo la Mhehsimiwa Naibu
Waziri, na mpaka sasa hivi tatizo la maji kwa maeneo ya Pangani Mjini tunalifanyia
kazi kwa maana mashine ambayo tunaitegemea kuitumbikiza katika kisima ambacho
kimeleta shida ipo katika hatua za mwisho za matengenezo, kwa hivyo tunategemea kwa siku ya kesho
itakuwa imekamilika matengenezo hayo, na pia tunaomba radhi kwa usumbufu unao
jitokeza kwa sasa.’’ Alisema Bwana Adamu
Mapema jana Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji
Jumaa Awesso alitoa agizo kwa mamlaka hiyo wilayani Pangani kufanya matengenezo ya haraka
ili kuondoa usumbufu uliojitokeza wa kukosa maji kwa wakazi wa Pangani Mjini.
No comments