PANGANI YAJADILI JINSI YA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA (SIKU 16 ZA UKATILI WA KIJINSIA)

Mjadala wa katika kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia umefanyika leo katika jengo la Pangarithi huku ukiwashirikisha wadau kutokea taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali wilayani Pangani.

Mjadala huo umefanyika ukiwa na lengo la kutambua juhudi za wadau katika kupambana na ukatili wa kijinsia wilayani humo, ambapo wadau kutoka ofisi ya mkuu wa wilaya, jeshi la polisi wilaya, TAKUKURU, Ustawi wa Jamii, Afya na wananchi walipata nafasi ya kutoa maoni yao.

Mjadala huo ambao umeratibiwa na shirika la UZIKWASA sambamba na Pangani FM, umeonekana kuwa chachu ya kutokomeza ukatili wa kijinsia baada ya washiriki kuibua suala la mkwamo wa kutoa ushahidi pindi panapotokea matukio kama hayo.
Mjadala huo umetoa fursa kwa wanawake, wanaume, vijana wa kike na kiume na wanaharakati wengine kukuza uelewa juu ya mchango wa wanawake katika maendeleo na kutafakari matokeo ya harakati za ukombozi wa mwanamke.

Siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia ni kampeni  ya Kimataifa  inayoongozwa na Kituo cha Kimataifa cha wanawake katika uongozi tangu mwaka 1991.

Chimbuko la siku 16 za kupinga unyanyasaji wa kijinsia imetokana na mauaji ya kinyama ya wanawake wa eneo la Mirabelle yaliyofanyika nchini Dominica mwaka 1960.

Mwaka 1991 Umoja wa Mataifa (UN) ulichagua Novemba 25 iwe siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia ambapo kilele chake huadhimishwa Desemba 10 ya kila mwaka, ambapo kwa mwaka huu imebeba kauli mbiu isemayo "Funguka! Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto Haumuachi Mtu Salama"

No comments

Powered by Blogger.