VMAC YA KIJIJI CHA MSARAZA WILAYANI PANGANI YATOA MSAADA
Kamati ya kudhibiti Ukimwi,
Jinsia na Uongozi ya kijiji cha Msaraza imepongezwa kwa kazi ya kutoa elimu,
kuchangia chakula pamoja na kuhamasisha jamii katika shughuli za kimaendeleo
katika kijiji chao.
Akizungumza na wananchi
waliohudhuria tamasha lililoandaliwa na wajumbe wa VMAC wa kijiji hicho mgeni
rasmi Bwana Daudi Mlahagwa ambae ni kaimu mkurugenzi wilaya ya Pangani
amesema kamati hiyo imefanya kazi
kulingana na mafunzo waliyoyapokea kutoka shirika la UZIKWASA.
‘’Kuna mambo mengi sana
ambayo mnayafanya vimac ya kijiji hichi cha Msaraza, mmeweza kutoa elimu kwa
wanakijiji, mmeweza kutoa chakula kwa wanafunzi wa shule, mmeweza kuhamasisha
jamii kwa ajili ya ushiriki wao katika shughuli za maeneleo, na kupiga vita
unyanyapaa na maambukizi ya ukimwi lakini naamini haya yote ni kwa kushirikiana
na shirika la uzikwasa pia nichukuwe fursa hii kulipongeza shirika hili kwa
kazi nzuri ya kuzipa nguvu kamati za vimac.’’ Mlahagwa.
Kwa upande wa madiwani
waalikwa kwenye Tamasha hilo Mheshiwa John Semkande pamoja na Bi Samira Kassim wamesema
wako tayari kuiunga mkono kamati hiyo pamoja na kumtaka mkurugenzi wa
halmashauri kuwashika mkono katika shughuli za kimaendeleo.
‘’jamani nafarijika sana kwa
sababu mwenyekiti mwenzangu wa kijiji ni wa chama cha demokrasia na maendeleo
kwa hiyo niwaambie tu kwamba maendeleo hayana chama, kwa hilo tutaungana na
nyinyi kwa kutoa zawadi ya mbuzi mmoja’’ amesema Mheshimiwa Semkande.
Naye katibu wa kamati hiyo Bwana
Iddi Waziri Mazika amesema kuwa wametoa zawadi kwa watoto yatima wazee na bima
kwa wanafunzi 60 wa shule za msingi.
‘’Kutoa zawadi kwa wazee kumi kwa kuwapa unga, na tumetoa zawadi kwa
watoto yatima wawili ya mbuzi kwa kila mototo mbuzi wake, tumetoa zawadi kwa
watoto 60 wa shule ya msingi bushiri ya bima ya afya ambayo inamaliza muda wake
mwaka 6/12/2018’’. Amesema Mazika.
Licha ya kufanya tamasha hilo
kwa kugawa zawadi kwa wanafunzi watoto
yatima na kuwasaidia wazee wa kijijini hapo, tamasha hilo pia liliambatana na
upimaji wa hiyari wa VVU ambapo katibu huyo amewapongeza kwa kwa uamuzi wao wa
kupima kwa hiari.
No comments