WAKULIMA PANGANI WATAKIWA KUFUATA USHAURI WA KITAALAMU
Wakulima wilayani Pangani wametakiwa kuzingatia
ushauri wa wataalamu wa kilimo ili kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya
tabia ya nchi na kuongeza thamani ya mazao.
Akizungumza na Pangani Fm afisa kilimo wa kata ya
MADANGA Bwana Rajabu Kiroka mbali na
kuwataka wakulima kuzingatia ushauri wa kitaalamu, amewashuri kutumia mbegu
zinazokomaa kwa muda mfupi na kuwataka wafugaji kupunguza mifugo yao ili iweze
kuwa na tija.
‘’Ninachowashauri wakulima kwanza wawe bega kwa
began a wataalamu wa kilimo kwa kuwa pamoja na kusikiliza ushauri wa wataalamu
kwa kupanda mbegu bora, na kwa wale wafugaji wafuge kwa kutumia ufugaji wa
kisasa kwa maana ya kuwa na idadi ndogo ya mifugo ili kuepusha migogoro ya
wafugaji’’ Amesema Kiroka.
Kwa upande wake mkulima katika kijiji cha madanga
ameeleza kuwa changamoto kubwa ya mabadiliko hayo yanatokana na uharibifu wa
mazingira ikiwemo suala la ukataji miti hovyo.
‘’Kiukweli ukataji wa miti umeshamiri sana hasa kwa
kata yetu ya madanga na wazee wetu wametuachia minazi lakini hadi sasa
imemalizika kabina watu wanakata miti ovyo bila ya kuangalia athari ya baadae
ni nini kwa kweli lazima serikali itoe elimu ili kukabiliana na mabadiliko ya
tabianchi’’ Amesema Arabia.
Mabadiliko ya tabia nchi yamekua miongoni mwa ajenda
kuu katika jumuia mbali mbali za
kimataifa ikwemo umoja wa mataifa na jumuiya ya afrika na inasadikiwa kila
mwaka watu zaidi 200 huathiriwa na ukame mafuriko ambayo ni matokeo ya
mabadiliko ya tabia nchi.
No comments